0 00:00:01,15 --> 00:00:03,18 Nafasi na Cheo cha mjuzi wa A`al Muhammad, Imam Aliy bin Mussa Al_Ridha (a.s) 1 00:00:05,02 --> 00:00:06,16 Mawaidha ya Ayatullah Al_udhmaa Wahiid Khorasani 2 00:00:07,18 --> 00:00:10,12 Jumatano 9 / 1430 Hijria Qamariy = 6 /6 /1388 Hijria Shamsiy 3 00:00:11,07 --> 00:00:16,19 Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu 4 00:00:17,14 --> 00:00:55,13 Kila sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa viumbe na Sala za Mwenyezi Mungu zimfikie Bwana Muhammad na jamaa zake waliotakasika hasa Imam Zamani na laana ziwashukie maadui zake hadi siku ya malipo. 5 00:00:56,08 --> 00:01:03,12 Somo letu lilikuwa katika herufi za alfabeti za Qur`ani - abjadi 6 00:01:04,03 --> 00:01:10,12 na somo halikuisha (hata) katika Alif; 7 00:01:10,20 --> 00:01:21,11 lakini leo kwa sababu wengi wanataka 8 00:01:22,05 --> 00:01:39,00 tuzungumzie kuhusiana na Imam Aliy bin Mussa (a.s), 9 00:01:39,14 --> 00:01:52,00 ijapokuwa mada hii ni ngumu, lakini tutajitahidi kwa kadri tutakavyojaaliwa … 10 00:01:52,05 --> 00:02:00,09 kuzungumza kuhusu yeye, ni (sawa) na kuzungumza uhakika wa Qur`ani. 11 00:02:00,15 --> 00:02:06,23 Majlis pia ni majlis ya Qur`ani. 12 00:02:07,04 --> 00:02:21,13 ijapokuwa kumjuwa Hazrat huyo iko nje ya uwezo wetu! 13 00:02:24,19 --> 00:02:31,17 wakati Imam wa nane atakapo fahamika 14 00:02:32,15 --> 00:02:44,17 basi ubinadamu na ukamilifu wa binadamu pia utafahamika. 15 00:02:50,01 --> 00:02:58,14 wakati huo atafahamika (kuwa) yeye ni nani 16 00:02:58,21 --> 00:03:10,24 anaweza kuufikisha ulimwengu katika malengo ya mwisho na ya juu. 17 00:03:11,05 --> 00:03:24,13 ulimwengu huu na vilivyomo vyote, ni utangulizi wa maisha; 18 00:03:24,20 --> 00:03:35,16 kuifahamu Qur`ani kuna ugumu (mkubwa)! 19 00:03:35,23 --> 00:03:48,21 ((Tutawaonyesha dalili zetu katika ulimwengu na katika nafsi zao)); 20 00:03:49,01 --> 00:03:58,15 huyu ni binadamu katika upande mmoja wa mizani, na 21 00:03:58,19 --> 00:04:04,13 na ulimwengu katika upande mwengine wa mizani. 22 00:04:08,20 --> 00:04:18,00 huu ni utangulizi mtukufu na adhimu, 23 00:04:18,04 --> 00:04:23,12 mpaka tufike kwa mwenye utangulizi mwenyewe! 24 00:04:23,17 --> 00:04:34,01 kisha huyo mwenye utangulizi akufikishe katika malengo ya mwisho. 25 00:04:39,05 --> 00:04:58,12 katika Qur`ani tukufu, neno ((Tabaraka)) limekuja karibu mara tisa; 26 00:04:58,16 --> 00:05:07,20 lakini kila mara limekuja kwa upana wake ukubwa ambapo 27 00:05:08,00 --> 00:05:18,02 kuingia katika mada hii kuna ugumu sana! 28 00:05:18,23 --> 00:05:24,24 mfano wa jambo hilo ni: 29 00:05:25,04 --> 00:05:35,08 sura mbili katika Qur`ani, lakini ni sura zipi hizo! 30 00:05:36,06 --> 00:05:42,00 hilo pekee lina maelezo mengi na ni somo pana 31 00:05:42,03 --> 00:05:54,14 moja ni surat Furqan; na nyengine ni surat Mulk. 32 00:05:54,16 --> 00:06:08,18 wale ambao ni watu wa kuzingatia na kufikiria, basi basi wende wakatwalii, 33 00:06:08,21 --> 00:06:20,11 wataona katika surat Mulk kuna habari gani, katika kila aya! 34 00:06:23,15 --> 00:06:29,08 katika surat Furqan kuna habari gani! 35 00:06:29,12 --> 00:06:39,04 kila moja katika sura hizi inaendana na aya. 36 00:06:39,08 --> 00:06:47,23 na kila moja ya aya hizi mbili, basi zinaendana na neno ((Tabaraka)). 37 00:06:48,02 --> 00:06:56,16 neno ((Tabaraka)) Mwenyezi Mungu amelizungumza wapi? 38 00:06:59,20 --> 00:07:11,15 ((Mwenye baraka ni yule aliyeteremsha Qur`ani kwa mja wake 39 00:07:11,19 --> 00:07:18,02 ili awe muonyaji kwa walimwengu)). 40 00:07:22,05 --> 00:07:32,09 katika wakati huu finyu, na mazungumzo ya kumjua Imam wa nane, 41 00:07:32,13 --> 00:07:43,22 itawezekana vipi kwa mat-labu hii, mpaka kufikia kiwango cha msingi (base)?! 42 00:07:45,13 --> 00:07:57,18 katika surat Mulk, ((Kwa Jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu, 43 00:07:58,04 --> 00:08:05,10 Ametukuka yule ambaye mkononi mwake umo ufalme 44 00:08:05,15 --> 00:08:11,19 naye ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu, 45 00:08:12,15 --> 00:08:18,05 ambaye ameumba kifo na uzima )) 46 00:08:18,16 --> 00:08:23,17 kisha kuna habari mzito na kiyama! 47 00:08:26,23 --> 00:08:32,09 ukifikia jinsi alivyoumbwa mwanadamu, 48 00:08:32,23 --> 00:08:39,13 inaelezea marhala na hatua (viza) saba vya kuubwa mwanadamu. 49 00:08:39,17 --> 00:08:52,19 mwanadamu kama bado hajafahamika, basi Imam Ridha hawezi kufahamika. 50 00:09:00,00 --> 00:09:06,03 mwanadamu ana hatua (viza) saba; 51 00:09:10,08 --> 00:09:17,15 marhala ya kwanza inaanzia kutoka 52 00:09:17,19 --> 00:09:28,06 ((Na bila shaka tulimuumba mwanadamu kutokana na asli ya udongo)); 53 00:09:28,14 --> 00:09:39,08 marhala ya saba: ((kisha tukamfanya kiumbe kingine)). 54 00:09:39,13 --> 00:09:51,14 inaendelea katika marhala ya saba: ((Basi ametukuka Mwenyezi Mungu, mbora wa waumbaji)). 55 00:09:51,22 --> 00:10:04,04 hivi ndivyo jinsi ilivyotumika ((Tabaraka)); 56 00:10:04,09 --> 00:10:10,18 ile ((Tabaraka)) iliyoko katika surat Mulk, na 57 00:10:10,22 --> 00:10:16,08 na ile ((Tabaraka)) katika surat Furqan, na 58 00:10:16,12 --> 00:10:28,05 na ile ((Tabaraka)) katika surat Muuminuuna, ni lazima zijumlishwe. 59 00:10:32,08 --> 00:10:36,23 hapa Mwenyezi Mungu anasema: 60 00:10:37,03 --> 00:10:42,08 ((basi ametukuka Mwenyezi Mungu, mbora wa waumbaji)); 61 00:10:42,12 --> 00:10:45,23 huyu ndiye mwanadamu! 62 00:10:46,02 --> 00:10:55,16 sasa, ukamilifu wa mwanadamu upo katika nini? 63 00:10:55,19 --> 00:11:03,05 ukamilifu wa mwanadamu unapatikana kwa maneno mawili; 64 00:11:03,09 --> 00:11:15,14 ni maneno mawili kwa hesabu: moja ni Akili; na nyengine ni Imani. 65 00:11:15,18 --> 00:11:25,04 mwili huu umejengeka kwa akili na nakili: 66 00:11:25,09 --> 00:11:31,19 ukamilifu wa kuubwa ni: mwanadamu. 67 00:11:32,16 --> 00:11:36,18 ukamilifu wa mwanadamu ni : Akili na Imani. 68 00:11:36,23 --> 00:11:42,15 Imam wa nane ana hadithi mbili: 69 00:11:42,17 --> 00:11:48,17 moja katika akili; na nyengine katika imani 70 00:11:48,21 --> 00:11:58,12 katika kila hadithi, na katika kila sentensi, amepasua mwezi! 71 00:11:58,18 --> 00:12:04,16 wakati huo , atafahamika Imam wa nane! 72 00:12:04,20 --> 00:12:21,07 Ibn Sikkit mtu ambaye Ibn Khalkaan, kuhusiana na kitabu chake, ameandika: 73 00:12:21,10 --> 00:12:34,00 hiki ni kitabu ambachi hakina mfano, na ni kitabu cha Murajaa kwa wote. 74 00:12:37,03 --> 00:12:47,24 mtu kama huyo akaja [kwa Imam] na kupiga magoti chini ya ardhi, na kusema: 75 00:12:48,03 --> 00:12:54,19 ewe mtoto wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Hojat, leo kuna nini? 76 00:12:54,24 --> 00:12:59,24 akasema: ((Akili)). 77 00:13:00,02 --> 00:13:05,17 hawa ni watu ambao wanafahamu kwamba 78 00:13:05,21 --> 00:13:15,15 elimu zote ni akili, philosophy ya nadharia, na philosophy ya matendo 79 00:13:15,18 --> 00:13:23,06 kuanzia mwanzo mpaka mwisho amezifatiliza , na kuzichambua, 80 00:13:23,10 --> 00:13:30,22 kisha anaelewa yeye kwa Sikkit alimwambia vipi! 81 00:13:31,02 --> 00:13:37,05 alisema: Akili ni Hojat. 82 00:13:37,08 --> 00:13:46,01 kisha katika maelezo mengine, alielezea ukamilifu wa akili kwamba 83 00:13:46,13 --> 00:13:52,00 ukamilifu wa akili upo katika kitu gani? 84 00:13:52,06 --> 00:14:00,15 haya ni lazima muyaelewe, wakati huo alielewa kuwa 85 00:14:00,18 --> 00:14:06,15 dunia imeharamishiwa elimu na mafunzo gani! 86 00:14:06,19 --> 00:14:16,14 akasema: akili ya mtu haimaliziki isipokuwa kwa mambo haya; 87 00:14:16,18 --> 00:14:24,03 sisi tutazungumza muhtasari na sehemu moja kati ya hizo. 88 00:14:24,06 --> 00:14:29,23 Moja, ((katika kheri kuna matumaini ….)). 89 00:14:30,01 --> 00:14:37,24 ameanza na neno gani?! 90 00:14:39,11 --> 00:14:44,20 sentensi yake ya kwanza inaanza na ((kheri)). 91 00:14:44,24 --> 00:14:57,23 hii ndio sababu kwamba kuelewa hadithi hii na fiqhi ya riwaya hii, bila ya ….. 92 00:14:58,04 --> 00:15:08,20 ((katika kheri kuna matumaini na katika shari kuna Uabbas-ufalme)). 93 00:15:13,24 --> 00:15:18,01 amechukuwa maneno mawili: Kheri na shari. 94 00:15:18,03 --> 00:15:26,22 ((Alif na Laam)) imekuja mbele ya kila neno, ((Alif na Laam )) jinsy. 95 00:15:27,00 --> 00:15:36,16 jinsy ya kheri inatokana na matumaini; 96 00:15:36,18 --> 00:15:40,21 na jinsy ya shari inatokana na Uabbas-ufalme. 97 00:15:45,22 --> 00:15:52,13 tumesema: kila sentensi ina ufafanuzi mpana. 98 00:15:52,16 --> 00:15:59,19 Imam wa nane atafahamika kutokana na sentensi hizi. 99 00:15:59,22 --> 00:16:07,12 pili, anaziacha hizi mbili, 100 00:16:11,15 --> 00:16:23,06 wingi wa kheri mwenyewe anauhesabu kuwa ni kidogo (si kitu); ama 101 00:16:23,10 --> 00:16:29,12 uchache wa kheri kwa wengine anauhesabu kuwa ni wingi. 102 00:16:31,16 --> 00:16:40,11 kwa hivi ndio akili hufikia katika ukamilifu. 103 00:16:46,17 --> 00:16:56,17 yeye hawi ombaomba akataka kusaidiwa; 104 00:17:00,22 --> 00:17:18,17 waombaje wengi wanarejea kwake kuomba, kwa sababu yeye hakuwahipo kuomba. 105 00:17:18,21 --> 00:17:24,15 hii ni kuhusiana na viumbe; 106 00:17:24,18 --> 00:17:28,18 ama kuhusiana na yeye mwenyewe: 107 00:17:28,21 --> 00:17:53,01 ((hakutosheka na kutafuta elimu katika umri wake wote. 108 00:17:53,06 --> 00:18:00,23 amefanya nini katika kila sentensi! 109 00:18:01,05 --> 00:18:16,01 kisha akasema: kuwa faqiri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kwake kuliko utajiri; 110 00:18:16,05 --> 00:18:26,15 kuwa dhalili mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora kwake kuliko madaraka na nguvu. 111 00:18:30,21 --> 00:18:41,15 akijikweza hivi katika mwili wake wa kibinadamu, 112 00:18:41,19 --> 00:18:46,03 ((nguzo na muhimili wa mwanadamu ni akili)), 113 00:18:46,07 --> 00:18:54,11 hii iwache, ni lazima mkono huu ufike chini ya bustani ili upate matunda! 114 00:18:54,15 --> 00:19:02,18 hadithi iko wazi, mwisho wake tunasema; 115 00:19:02,23 --> 00:19:11,03 kwa sababu yeye mwenyewe ametosheka na kuridhika na neno la mwisho; 116 00:19:11,06 --> 00:19:16,10 alisema: ((Muashirat na nini Muashirat )) 117 00:19:16,15 --> 00:19:20,08 la mwisho ni hili: 118 00:19:20,13 --> 00:19:24,04 asimuone yeyote 119 00:19:24,08 --> 00:19:29,12 neno ((Ahad)) ni jinsi gani lilivyo kwa umumy! 120 00:19:29,17 --> 00:19:38,04 asimuone yeyote isipokuwa aweze kusema yeye ni bora kuliko mimi. 121 00:19:38,08 --> 00:19:44,24 wakati akifika hapa, basi akili hukamilika; 122 00:19:45,02 --> 00:19:51,01 kwa nini? Baadae atapambanua; 123 00:19:51,02 --> 00:19:58,18 kwa sababu kila atakayemuona, hatutoka katika moja ya hali mbili: 124 00:19:58,22 --> 00:20:03,15 aidha yeye ni bora kuliko wewe, au wewe ni bora kuliko yeye. 125 00:20:03,17 --> 00:20:14,19 yule ambaye si mbora kuliko yeye, wakati unapomfikia, 126 00:20:18,22 --> 00:20:32,21 anaona shari yake iko wazi (dhahiri), ama laiti kheri yangu ingekuwa ndani; 127 00:20:33,02 --> 00:20:39,11 lakini kuhusiana na wewe mwenyewe, kheri yako iko wazi (dhahiri). 128 00:20:39,16 --> 00:20:48,06 huenda ile kheri iliyo ndani(iliyojificha) iwe ni yenye kukubaliwa mbele ya Mwenyezi Mungu. 129 00:20:48,10 --> 00:20:58,21 na ile shari iliyo ndani mwako iwe ni sababu ya kukusahaulisha [na kukughafisha na maamrisho ya Allah] 130 00:20:59,18 --> 00:21:04,17 na ile kheri iliyo dhahiri pia ikawa ni yenye kukataliwa. 131 00:21:04,22 --> 00:21:14,17 wakati ikiwa hivi, basi ile shari kwangu ni bora. 132 00:21:14,23 --> 00:21:19,18 muhtasari wa maelezo haya ni kwamba: 133 00:21:19,22 --> 00:21:24,00 watu wa fani (wenye ustadi), 134 00:21:24,03 --> 00:21:29,11 kuhusiana na wenyewe basi hujiona hawana elimu, 135 00:21:29,15 --> 00:21:33,03 na kuhusiana na yeye huona hakuna elimu. 136 00:21:33,08 --> 00:21:41,13 kutokuwa na elimu na kuwa si elimu haya ni mambo yasiyoingiliana. 137 00:21:41,17 --> 00:21:46,09 wakati huo, akili hukamilika. 138 00:21:46,14 --> 00:21:51,01 ama ukiona ni bora, 139 00:21:51,05 --> 00:21:59,01 ni lazima umfate yeye ili uweze kufikia kila zuri. 140 00:21:59,05 --> 00:22:03,19 ikiwa hivyo, basi akili hukamilika. 141 00:22:03,23 --> 00:22:08,11 haya ni maneno yake katika ukamilifu wa akili. 142 00:22:08,15 --> 00:22:13,20 wakati akija kwa upande wa imani … 143 00:22:13,24 --> 00:22:20,05 nani aliyelala katika Toos - Mashahad?! Ni nani?! 144 00:22:20,08 --> 00:22:30,12 wakati inapofikia kwenye imani , anasema: 145 00:22:33,01 --> 00:22:41,23 muumini, haikamiliki imani yake isipokuwa awe ndani yake ana sunna tatu: 146 00:22:42,09 --> 00:22:55,03 moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu; pili kutoka kwa Mjumbe wa Allah, na ya tatu kutoka kwa Maimamu waongofu. 147 00:22:55,08 --> 00:23:00,18 ama kutoka kwa Mwenyezi Mungu (( Kuwa msitiri wa siri (za wengine) )). 148 00:23:00,24 --> 00:23:08,22 wakati muuminini, imani yake inapokamilika 149 00:23:09,00 --> 00:23:15,00 basi kujifunza kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msitiri wa siri; 150 00:23:20,03 --> 00:23:24,21 mbebaji wa siri. 151 00:23:25,00 --> 00:23:30,11 pia katika maneno haya kuna habari mzito! 152 00:23:31,02 --> 00:23:37,01 yaani ni siri gani anatunza kutoka kwa Mwenyezi Mungu?! 153 00:23:37,24 --> 00:23:44,01 ama kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ((kuwa na tabia njema)) 154 00:23:45,01 --> 00:23:48,03 amefanywa nini ? 155 00:23:50,06 --> 00:23:56,20 angalieni, amevunjwa jino lake, na 156 00:23:57,07 --> 00:24:01,18 na ametiwa uchafu katika kichwa chake, na 157 00:24:02,01 --> 00:24:06,14 yeye ni mtu wa kwanza duniani mwenye hadhi, 158 00:24:06,17 --> 00:24:16,00 na katika hali hiyo alifanya naye muamala, kisha akasema: 159 00:24:16,09 --> 00:24:21,22 ((Ewe Mola wangu waongoze watu wangu kwani kwa hakika si wenye kujuwa)). 160 00:24:22,05 --> 00:24:31,05 badala yake adhabu zote na shida alizopata kutoka kwa watu , basi aliwaombea dua, 161 00:24:31,12 --> 00:24:34,23 alitaka nini kwa Mwenyezi Mungu?! 162 00:24:35,03 --> 00:24:40,00 ((Ewe Mola wangu waongoze watu wangu)). 163 00:24:40,21 --> 00:24:44,09 kisha kiyama ni hivi : 164 00:24:44,14 --> 00:24:53,19 ukifuatilia (( Ewe Mola wangu waongoze … )) neno (( Qaumiy)). 165 00:24:53,23 --> 00:25:05,10 watu hao wa bara Arabu alijinasibisha nao, ili kuwaombea msamaha wa adhabu. 166 00:25:05,14 --> 00:25:14,14 kisha kile ambacho kinashangaza akili ni kwamba 167 00:25:14,19 --> 00:25:22,23 mwisho aliwaombea msamaha na udhuru; 168 00:25:24,01 --> 00:25:31,18 alileta sababu, alisema: ((Kwa hakika si wenye kujuwa)); 169 00:25:32,09 --> 00:25:40,22 wasamehe kwani wao si wenye kujuwa (majahili). Ukubali udhuru wao. 170 00:25:41,05 --> 00:25:49,10 kuchuwa vigezo hivi; wakati huo utakuwa muumini. 171 00:25:49,17 --> 00:25:58,18 ama kutoka kwetu; (( kuwa mvumilivu na mwenye subira katika misiba na majanga)). 172 00:25:58,23 --> 00:26:09,09 kwa maneno haya matatu, basi mwanadamu anaweza kufika katika malengo ya juu. 173 00:26:09,15 --> 00:26:20,11 Maulamaa wote wa akhlaq, kuanzia zama za Arastwuu mpaka sasa, 174 00:26:20,16 --> 00:26:37,23 kile ambacho watu wa elimu ya hadithi (Rijaliy) wameweza kukifanyia kazi katika kumlea na kumnowa mwanadamu, ni marhala tatu: 175 00:26:38,03 --> 00:26:42,15 marhala ya kwanza: kwenda chooni; 176 00:26:42,19 --> 00:26:50,18 marhala ya pili: uchambuzi; 177 00:26:50,20 --> 00:26:54,24 marhala ya tatu: uvumilivu. 178 00:26:55,04 --> 00:27:04,05 marahala zote tatu zimekusanywa katika riwaya mbili! 179 00:27:04,09 --> 00:27:15,06 na pia mapungufu yote yaliyomo katika hekmat ya matendo yameondolewa kwa riwaya mbili! 180 00:27:15,12 --> 00:27:25,19 ikiwa maneno yake yatafanyiwa utafiti, na kushereheshwa, na 181 00:27:25,24 --> 00:27:32,13 yakafahamika, na yakafanyiwa kazi kwa matendo, 182 00:27:32,17 --> 00:27:38,14 hadithi zake mbili zinaweza kubadilisha dunia mzima! 183 00:27:46,19 --> 00:27:54,12 je kumjuwa mtu kama huyu ni rahisi?! 184 00:27:54,15 --> 00:28:11,11 riwaya hii Alliy bin Ibrahim kutoka kwa Ibrahim bin Hashim, 185 00:28:12,09 --> 00:28:23,02 yeye ameipokea kutoka kwa Ibn Abi Amiri, na Ibn Abi Amiri kutoka kwa baadhi ya Masahaba wake 186 00:28:23,07 --> 00:28:31,07 kutoka kwa Omar bin Yazid kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) … 187 00:28:36,11 --> 00:28:42,24 riwaya kama hii! Yenye sanadi hii! 188 00:28:43,05 --> 00:28:57,23 Imam amesema: Hija moja ni sawa sawa na kuwachia huru watumwa sabiini. 189 00:28:58,08 --> 00:29:04,20 kisha, Omar bin Yazid … 190 00:29:05,00 --> 00:29:10,16 watu ambao ni wanafiqhi, wanawafahamu wapokezi. 191 00:29:10,21 --> 00:29:20,09 katika ufaqihi ni lazima nukta hii, kufahamu mpokezi ni nani. 192 00:29:20,14 --> 00:29:31,14 Omar bin Yazid, Muawiya bin Ammar, Zurarah, Abu Baswiir. 193 00:29:31,18 --> 00:29:38,00 aliuliza: jee kuna kitu chochote kilichosawa na (thawabu za ) Hija? 194 00:29:38,05 --> 00:29:46,18 Imam akasema: Hakuna kitu chochote kilichosawa na Hija. 195 00:29:46,23 --> 00:30:09,01 dirhamu moja katika njia ya Hija ni sawa sawa na dirhamu elfu mbili zisizokuwa kwa njia ya Hija kwa njia ya Allah. 196 00:30:09,08 --> 00:30:14,04 riwaya hii ihifadhini vizuri. 197 00:30:14,10 --> 00:30:25,14 Masheke watatu, Yaani Theqatul Islamu Kulayniy, 198 00:30:25,18 --> 00:30:31,10 Sheikh Twaifah katika Tahziib, 199 00:30:31,16 --> 00:30:38,12 Sheikh Swaduq katika Ghuyuun na katika Amaal, 200 00:30:38,16 --> 00:30:48,04 imenakiliwa riwaya ambayo masheikh watatu wamekubaliana …. 201 00:30:48,11 --> 00:30:52,18 baadhi ya sehemu ya riwaya ni hii: 202 00:30:52,23 --> 00:31:07,01 Imam wa saba amesema: Kumzuru baba yangu Alliy …. 203 00:31:07,05 --> 00:31:10,17 zingatieni kwa makini. 204 00:31:11,14 --> 00:31:26,06 Kumzuru baba yangu, Alliy ni bora kuliko Hija sabiini Mabrura! 205 00:31:26,11 --> 00:31:34,03 Hija kama hiyo, na utukufu wake huo! 206 00:31:34,08 --> 00:31:46,22 Ziyara yake moja inakuwa sawa sawa, kama itawekwa katika upande mmoja wa mizani, 207 00:31:47,01 --> 00:31:53,18 na Hija sabiini Mabrura, nayo sio kila Hija! 208 00:31:53,23 --> 00:31:57,24 hii ni sentensi ya kwanza. 209 00:32:01,03 --> 00:32:10,21 kutokana na ((Inna)), yaani kutoka kwa athari inakwenda kwa muathiri. 210 00:32:10,24 --> 00:32:22,05 kisha jambo hili halikuishia hapa; akasema: 211 00:32:23,02 --> 00:32:38,11 mtu ambaye atamzuru yeye, usiku mmoja aupitishe kwenye kaburi lake, 212 00:32:38,15 --> 00:32:46,03 ((anakuwa ni sawa sawa na aliyemzuru Allah katika arshi yake)). 213 00:32:46,08 --> 00:32:56,19 maelezo haya yanatoka kwa mtu ambaye ana dhamana ya utoharifu kutoka kwa Mwenyezi Mungu! 214 00:32:56,24 --> 00:33:03,21 ((anakuwa ni sawa sawa na aliyemzuru Allah katika arshi yake)). 215 00:33:04,00 --> 00:33:11,13 marhala nyengine, akasema: 216 00:33:11,18 --> 00:33:24,13 wakati itakaposimamishwa arshi ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, watu nane, 217 00:33:24,18 --> 00:33:33,14 watu wanne wa mwanzoni, na wanne wa mwishoni. 218 00:33:33,18 --> 00:33:45,01 wa mwanzoni: Nuhu, Ibrahim, Mussa, na Issa; 219 00:33:45,04 --> 00:34:00,10 mwa mwishoni: babu yake (Mtume), Amiril Muuminiina, Hassan bin Alliy, na Hussein bin Alliy. 220 00:34:02,12 --> 00:34:04,16 hii yenyewe ina siri! 221 00:34:05,04 --> 00:34:08,14 baada ya sententensi hii, alisema: 222 00:34:08,24 --> 00:34:27,03 Wazuruji wa makaburi ya Maimamu watakuwa pamoja na Maimamu wenyewe; 223 00:34:27,10 --> 00:34:47,04 ama ((wana nafasi za juu, na nafasi ya karibu zaidi ni ya mwenye kuzuru kaburi la baba yangu Alliy !)). 224 00:34:47,22 --> 00:34:49,22 huyu ndiye Imam Ridha (a.s)! 225 00:34:50,07 --> 00:35:04,19 huyu ndie Imam Ridha(a.s) ! ((wana nafasi za juu)) na nafasi ya karibu zaidi ni ya mwenye kuzuru kaburi la Alliy bin Mussa!. 226 00:35:05,01 --> 00:35:12,01 Imam wa nane kumuelezea kwake iko nje ya upeo wa mwanadamu! 227 00:35:12,10 --> 00:35:17,14 sasa kuna vigezo gani vya kipekee ndani yake? 228 00:35:17,19 --> 00:35:21,04 mwisho wa mat-lab, 229 00:35:21,07 --> 00:35:26,15 kwa sababu watu ni lazima wafahamu kuna habari gani. 230 00:35:26,20 --> 00:35:40,24 inasikitisha kuwa hatufahamu! Hatujuwi nchi hii iko chini ya mikono ya nani! 231 00:35:45,05 --> 00:35:50,08 salamu (Salawat) zako zote unazozituma 232 00:35:50,13 --> 00:35:53,02 katika salamu unazemaje? 233 00:35:58,08 --> 00:36:02,14 A`al Muhammad ni kina nani? 234 00:36:02,21 --> 00:36:04,19 zingatieni kwa makini. 235 00:36:05,00 --> 00:36:08,04 wakati huo hadithi ni hii: 236 00:36:08,08 --> 00:36:21,04 Imam wa sita, kiongozi na raisi wa madhehebu, anamwambia mwanawe Imam wa saba: 237 00:36:21,09 --> 00:36:26,08 baada yako kuna Mjuzi wa A`al Muhammad! 238 00:36:32,17 --> 00:36:36,16 wakati mwengine husemwa Mjuzi wa watu, 239 00:36:36,23 --> 00:36:42,17 wakati mwengine husemwa Mjuzi wa Twaifah fulani; 240 00:36:42,22 --> 00:36:45,03 ama taabiri ni hii: 241 00:36:45,08 --> 00:36:52,15 kwa kweli taabiri hii inashangaza akili! 242 00:36:52,20 --> 00:37:01,00 sentensi yake ya pili inashangaza zaidi! Na sentensi yenyewe ni hii: 243 00:37:01,04 --> 00:37:07,13 mtu ambaye hatamani chochote isipokuwa kuwa karibu na Mwenyezi Mungu … 244 00:37:07,18 --> 00:37:14,20 mtu ambaye amefikia sehemu kwamba 245 00:37:15,03 --> 00:37:26,11 katika ((Wewe tu tunakuambudu, na kwako tu tunataka msaada)) aliisema mara nyingi mpaka akamsikia Mwenyezi Mungu 246 00:37:26,15 --> 00:37:32,01 mtu kama huyu alimwambia mwanawe sentensi hii … 247 00:37:32,07 --> 00:37:37,15 fikrieni kwa jinsi mutakavyoweza! 248 00:37:37,20 --> 00:37:52,20 249 00:37:53,01 --> 00:38:03,17 Sala na amani za Mwenyezi Mungu zimfikie Walii wako na Hujat wako Alliy bin Mussa Al_Ridha 250 00:38:03,22 --> 00:38:09,08 kwa idadi ile iliyomo katika elimu yako. 251 00:38:09,12 --> 00:38:17,22 sala ambazo zitadumu kwa kudumu ufalme wako na usultwani wako .